Sunday 29 December 2013

HOJAJI

KANUNI ZA UUNDAJI WA HOJAJI
Makala haya yanahusu kanuni za uandaaji wa hojaji. Katika kujadili mada hii tumegawa kazi hii katika sehemu tatu muhimu, sehemu ya kwanza fasili ya hojaji kulingana na wataalam mbalimbali, sehemu ya pili ni kiini cha swali ambapo inaelezea kanuni muhimu za uundaji wa hojaji, hatimaye hitimisho.
Kwa mujibu wa Kothari C.R, (2004),  uk 100, anafasili neno hojaji kuwa ni maswali yanayoandikwa katika karatasi ili yaulizwe kwa mtafitiwa kwa lengo la kupata taarifa za tatizo la utafiti.
Nayo Kamusi ya Kiswahili sanifu (2004) TUKI uk 116, inasema kwamba hojaji ni
karatasi yenye maswali ya uchunguzi.

Ni seti ya maswali mengi apewayo mtu/watu kwa lengo la kupata taarifa juu ya jambo fulani (Macmillan Dictionary) [1]
Kutokana na fasili hizo hapo juu tunaweza kusema kuwa, hojaji ni maswali yanayoandaliwa na mtafiti kwa lengo la kukusanya data kutoka kwa watafitiwa. Hojaji hizo mtafiti anaweza kupeleka mwenyewe kwa mtafitiwa kwa njia ya mkono au kwa njia ya posta ikiwa na kimbatanisho cha kumwomba mtafitiwa asome na kuelewa maswali kisha ajibu maswali katika nafasi zilizoachwa wazi kwa matumizi tu ya hojaji kisha kuyarudisha kwa mtafiti.

Hojaji zinazopelekwa kwa njia ya mkono husambazwa kwa haraka zaidi, na huwafikia watu wengi hususani wale wanaomzunguka mtafiti. Faida yake ni rahisi kukusanya, pia zinachukua muda mfupi, vilevile gharama zake ni ndogo,
Faida ya kutumia njia ya posta ni pamoja na kutumia gharama ndogo na husambazwa katika eneo kubwa kwa muda mfupi. Pia mtafitiwa ana muda wa kutosha wa kuweza kutoa majibu kadri maswali yalivyoulizwa. Pia mtafitiwa ambaye hawezi kuingiliwa kwa urahisi hii inaweza kuwa njia nzuri ya kutumia.
Licha ya njia hizo kuwa na faida pia zina hasara kama zifuatazo; kwanza mara nyingi hojaji zinazorudi zikiwa zimejazwa ni chache. Hii ni kutokana na mtafitiwa kutokuona umuhimu wa hojaji au kusongwa na majukumu au maswali kutokueleweka. Pili inabagua maana inahitaji watu wanaojua kusoma na kuandika, hojaji zinaweza kupotea zinapokuwa zinatumwa au kurudishwa. Ni vigumu kuelewa kama majibu yatolewayo ni ya kwa kweli au ya uongo.
Hata hivyo njia hii ni ya taratibu mno kuliko njia zingine katika ukusanyaji wa data.
Hojaji zimegawanyika katika makundi makubwa mawili; kwanza hojaji funge na hojaji za wazi (zisizo funge).
Hojaji funge maswali yake yako wazi na yanaeleweka kwa watafitiwa. Maswali yanayoulizwa yanakuwa sawa kwa watafitiwa wote, yanalenga kutoa jibu moja tu. Mfano ndiyo au hapana, au ya kuchagua a,b,c,d…. hayaruhusu mtafitiwa kuweka hisia zake. Muundo wa maswali waweza kuwa funge.
Kwa mfano; ANDIKA “N” KAMA JIBU NI NDIYO NA “H” KAMA JIBU NI HAPANA. AU CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHII TU.
Hojaji isiyo funge ni hojaji ambayo inamruhusu mtafitiwa kutoa maelezo/kujieleza/au kutoa maoni ya ziada (kutoa ufanuzi zaidi kadri ya uelewa wake kulingana na jinsi alivyoulizwa)
Hojaji kama njia ya ukusanyaji data ina kanuni muhimu za kuzingatiwa wakati wa kuiandaaa. Mtafiti hana budi kuzingatia mambo yafuatayo; kwanza; ajue TATIZO LA UTAFITI.
Mtafiti akishajua tatizo la utafiti itamsaidia kuandaa hojaji yake katika muundo unaotakiwa. Kwa mfano; atajua ni eneo gani ataenda kufanyia utafiti wake, umri wa watafitiwa, jinsia na kiwango chao cha elimu.
Tatu izingatie usuli wa watafitiwa kama vile jina, umri jinsia, kabila na kiwango cha elimu. Hii inasaidia mtatifi katika uchambuzi wa data kujua amehoji watu wa umri gani na amehoji watu wa kiwango gani cha elimu.
Pili ni mtiririko mzuri wa maswali; ili kutengeneza/kuandaa hojaji nzuri na kupata majiu sahihi mtafiti lazima azingatie mtiririko mzuri wa uaandaaji wa maswali. Mtiririko mzuri unaondoa uvulivuli/ukakasi kwa mtafitiwa, hivyo basi maswali lazima yawe katika mtiririko ufuatao;

  1. Kuanzia maswali mepesi kwenda maswali magumu, hii itampa moyo mtafitiwa au kumvutia na kuonesha ushirikiano lakini pia yatamvutia na kumpa moyo hivyo ataonesha ushirikiano au kupata hamasa ya kutaka kutoa majibu zaidi.
  2.  Maswali hayo yawe na uhusiano/ muwala.
      Maswali yafuatayo hayana budi kuekwa;
  1. maswali yanayomtaka mtafitiwa kufikiri sana
  2. maswali yanayomhusu mtafitiwa, mfano una watoto wangapi, mkewe yuko wapi, kwa         nini huna mtoto?
  3. Maswali yanayohusiana na mali za mtafitiwa, mfano je una magari mangapi? Au               unalipwa kiasi gani kwa siku?
Maswali yanayofuata baada ya maswali ambayo hayana budi kuepukwa ni maswali yanayohusiana na mada ya utafiti. Ambayo yanamtaka mtafitiwa kufikiri kiundani ili kuweza kutoa majibu sahihi.
Mfano, nafasi ya uchaguzi wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia elimu ya juu.
Maswali yalenge nini kinapelekea Kiswahili kuteuliwa kuwa lugha ya kufundishia elimu ya juu.
Au tatizo la utafiti ni watoto wa mtaani. Kwa hiyo maswali yalenge sababu za kuwepo watoto wa mitaani. Maswali magumu yaulizwe mwishoni. Hii ina faida kwa sababu, hata kama mtafitiwa atashindwa kujibu kutokana na sababu mbalimbali maswali yale ya awali yatakuwa yanatosha kutoa taarifa muhimu zinazohusu tatizo la utafiti.
Pia mtiririko wa maswali lazima uanze na maswali ya jumla kwenda maswali mahususi. Mtafitiwa hana budi kuelewa kuwa majibu yaliyotolewa ni kwa ajili ya utafiti huo.
jinsi/namna ya utungaji wa maswali hayo;
kutunga maswali katika mtiririko mzuri kwa kuanza na maswali rahisi kwenda magumu lakini pia kwa kuzingatia maswali ya jumla kwenda maswali mahususi. Maswali magumu yanaulizwa mwishoni.
Maswali yanayotungwa yawe wazi, yasiwe na upendeleo wa kijinsia au kisiasa au kidini. Maswali yazingatie vigezo vifuatavyo;
  1.  Maswali, yawe mafupi, yenye wazo moja, pia yawepo maswali ya majibu mafupi ya ndiyo au hapana, ya kuchagua na yawepo maswali ya kutoa maelezo.
  2. maswali yaeleweke/yawe sanifu
  3. maswali yaendane na uwezo wa kufikiri wa mtafitiwa, mfano unasuka kwa mwaka mara ngapi? Swali hilo ni gumu kwa maana hiyo lingeweza kuulizwa kuwa, kwa wiki unasuka mara ngapi? Hii itasaidia kufikiria kwa haraka.
Kanuni ya pili hojaji isiwe ndefu sana, na kila hojaji iwe na lengo moja tu. Matokeo ya hojaji kuwa ndefu itamchosha mtafitiwa. Muhimu maswali yasidokeze majiu.
Kwa mfano
            Hivi wewe ndo Honest?

            Hapa hospitali nasikia hakuna huduma nzuri ni kweli?
Tatu izingatie usuli wa watafitiwa kama vile jina, umri jinsia, kabila na kiwango cha elimu. Hii inasaidia mtatifi katika uchambuzi wa data kujua amehoji watu wa umri gani na amehoji watu wa kiwango gani cha elimu.
***namna/jinsi ya kutunga maswali, mtafiti lazima atambue kwamba kila swali lazima liwe wazi vinginevyo mtafitiwa hataelewa swali linataka nini. Vilevile maswali yasiwe na upendeleo wa kijinsia kwa mfano***
4.  Maswali yazingatie vigezo vifuatavyo; yawe rahisi, na yenye wazo moja la msingi. Maswali yaeleweke kirahisi. Maswali yaendane na uwezo wa kufikiri wa mtafitiwa mfano unasuka kwa mwaka mara ngapi? Swali hilo ni gumu kwa maana hiyo lingeweza kuulizwa kuwa kwa wiki unasuka mara ngapi? Hii itasaidia kufikiria kwa haraka.
Pamoja na hayo kuna miundo ya aina mbili ya utungaji wa maswali;
  1.  maswali yenye majibu ya kuchagua (funge)
  2. maswali yanayomruhusu mtafitiwa kujieleza (si funge)
FAIDA YA MASWALI FUNGE
Kwanza ni rahisi kujibu, yanaeleweka kwa urahisi, mtafitiwa ana uwezo wa kutofautisha swali moja na jingine
HASARA
Kwanza maswali hayo yanatoa majibu kwa mtafitiwa. Mfano Wahehe wanakula mbwa? Andika ndiyo au hapana, pia huzuia nafasi ya mtafitiwa kujieleza zaidi kwa jambo analolijua, pia hayako sahihi hasa pale ambapo yanakuwa magumu na hasa mtafiti anahitaji majibu sahihi.
Kutokana na udhaifu wa maswali funde, ndipo maswali ya wazi yanapohitajika.  
Maswali ya wazi yanatungwa kwatika mazingira ambayo yanatoa nafasi kwa mtafitiwa kutoa maelezo zaidi kwa kutumia maneno/maelezo yake binafsi.
FAIDA YA  MASWALI HURU
Huruhusu mtafitiwa kutoa maelezo mengi tena kwa maneno yake binafsi, mtafitiwa huwa huru katika kujieleza,.
HASARA
Ni vigumu kukabiliana nayo, kwa maana kwamba inaibua ugumu wa kubaini majibu sahihi ya swali lililoulizwa hii ni kwa sababu maelezo yanakuwa mengi. Pia mtafitiwa anaweza akawa na mtizamo hasi kwa hiyo akajibu ndivyo sivyo.
Kwa hakika hojaji nzuri haina budi kutumia njia zote mbili yaani njia ya maswali funge na njia ya maswali ya wazi. Kwani kwa kufanya hivyo unaweza kupata majibu ya ndiyo au hapana kadri ya maswali yaliyoulizwa, lakini pia utapata maoni mbalimbali na picha halisi kulingana na mtizamo wa mtafitiwa.
Mtafiti lazima awe makini katika maneno anayotumia katika kuaandaa maswali, maneno yawe na maana. Pia mtafiti lazima atumie sentensi rahisi. Maneno ambayo ni magumu ambayo hayaeleweke, istilahi za kitaalumaau na yenye maana zaidi ya moja lazima yaepukwe. Pia maneno ambayo hayaendani na utamaduni wa jamii husika lazima yaepukwe
Kimsingi utunzi wa maswali na utumiaji wa maneno ni sanaa ambayo inahitaji mtu kujifunza.



[1] http://www.macmillandictionary.com/dictionary/british/questinnair

4 comments:

  1. It was of great assistance

    ReplyDelete
  2. Baadhi ya maswali ya hojaji unapotafiti matumizi ya lugha ya sheng'

    ReplyDelete
  3. It's nice though I didn't find the content based on hojaji

    ReplyDelete